1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leicester City yakabiliwa na wakati mgumu

Bruce Amani
13 Februari 2017

Kocha wa klabu inayoyumba nchini England Liecester City Claudio Ranieri ameashiria kuwa yuko tayari kuwaweka benchi baadhi ya wachezaji walioshinda taji la Premier Premier msimu uliopita

https://p.dw.com/p/2XTfS
Fußball Leicester City Trainer Claudio Ranieri
Picha: Getty Images/M. Regan

Mabingwa hao hawajashinda mchuano – na hata kufunga bao – katika mechi sita za ligi mwaka huu, na walifungwa 2-0 na Swansea hapo jana. Sasa wako juu ya eneo la kushushwa daraja na pengo la pointi moja tu.

Ranieri amesema ni lazima afanye mabadiliko muhimu kwa sababu hawezi kuendelea kama ilivyo sasa. Wachezaji wao Jamie Vardy na Riyad Mahrez walikuwa moto wa kuotea mbali msimu ulioisha lakini msimu huu hawaonekana kutamba uwanjani.

Wakati hayo yakijiri, Chelsea iliijimarisha kileleni mwa ligi, kwa pengo la pointi kumi, licha ya kutoka sare ya 1-1 na Burnely. Nambari mbili Tottenham Hotspurs walilazwa mabao mawili kwa sifuri na Liverpool. Hata hivyo vita kamili ni vya kufuzu katika kandanda la Ulaya. ni pointi mbili tu zinazotenganisha Tottenham na nambari sita Manchester United. Arsenal ilishinda Hull mbili sifuri, na kusonga katika nafasi ya tatu juu ya Manchester City.

United walibakia katika nafasi ya sita licha ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Watford. Nambari tano Manchester City watacheza leo usiku dhidi ya Bournemouth na wataweza kupanda hadi nafasi ya pili kama watashinda.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu