1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LEIPZIG: Watu 100 wakamatwa mjini Leipzig

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6S

Polisi mjini Leipzig, mashariki mwa Ujerumani wamewakamata watu 100 wakati wa maandamano ya kupinga maandamano mengine ya manazi wa kileo, yaliyopangwa kufanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 16 ya muungano wa Ujerumani.

Mamia ya waandamanaji walivurumisha makombora, kuzifunga barabara na kuchoma motokaa ya polisi wa doria walipokuwa wakijaribu kuzuia mkutano wa hadhara wa manazi.

Maofisa takriban 200 wa polisi walikuwa na kibarua kigumu cha kuwalinda manazi, walioandamana katika barabara za mji wa Leipzig.

Hapo awali viongozi wa kisiasa katika eneo hilo, vyama vya wafanyakazi na makundi ya kidini, yalitoa mwito maandamano hayo yafanyike kwa amani.