1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LEIPZING: Kesi ya pili ya H5N1 yathibitishwa

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBo5

Maafisa wa afya nchini Ujerumani,wamethibitisha kuwa juma hili,kumegunduliwa kesi ya pili ya virusi hatari vya homa ya mafua ya ndege.Virusi aina ya H5N1 vimekutikana katika mabata maji watatu waliokufa karibu na mji wa Leipzig mashariki mwa Ujerumani.Hapo awali,virusi hivyo vilikutikana katika mizoga sita ya mabata maji, iliyogunduliwa siku ya Jumapili,umbali wa kama kilomita 200 kusini ya Leipzig.Wakuu wa afya wanalinganisha kesi hizo na zile za hivi karibuni nchini Hungary na Jamhuri ya Czech,ili kujua vipi virusi hivyo vimeingia Ujerumani.