1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni Marekani ama Japan

Halima Nyanza(ZPR)17 Julai 2011

Michuano ya kombe la dunia la soka la wanawake 2011, inamalizika leo hapa Ujerumani, kwa Marekani na Japan kupambana, kuwania ubingwa.

https://p.dw.com/p/11wqf
Baadhi ya wachezaji wa Marekani wakifurahia bao .Picha: picture-alliance/dpa

Marekani leo inajaribu bahati yake kuweza kunyakua kombe hilo kwa mara ya tatu, baada ya kufanikiwa kufanya hivyo mwaka 1991 na 1999.

Kwa upande wake, Japan ilipata ushindi wa kushangaza katika michuano hiyo, baada ya kuwatoa wenyeji na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Ujerumani.

Frauen Fußball WM Japanische Nationalmannschaft
Kikosi cha JapanPicha: AP

Jana Sweden iliweza kushika nafasi ya tatu ya michuano hiyo, baada ya kuifunga Ufaransa bao mbili kwa moja. Bao lake la ushindi lililofungwa na Marie Hammarström, lilipatikana dakika nane tu kabla ya mpira kumalizika.