1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuutokomeza umasikini duniani

17 Oktoba 2008

Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na umasikini duniani.Umoja wa mataifa umeiweka siku hii katika kuhamasisha jamii na serikali kupambana na umasikini.

https://p.dw.com/p/Fc8k
Umasikini Afrika: Mama na mtoto wake akisubiri kupata matibabuPicha: AP

Kwa mujibu wa azimio la wanaharakati wa haki za binaadamu lililopitishwa mnamo mwaka 1948 umasikini ni ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Na wakati dunia ikiadhimisha siku hii idadi kubwa ya watu bado wanaishi katika umasikini wa hali ya juu na kushindwa kukidhi mahitaji yao ya kila siku, wengi wakiwa ni kutoka katika nchi za dunia ya tatu.

Serikali na sekta binafsi zimekuwa katika harakati kubwa za kupambana na umasikini kwa njia ya kunyanyua uchumi wa nchi hizo.

Huko nchini Tanzania taasisi binafsi ya fedha inayohusika na mikopo ya easy finance imekuwa katika harakati hizo.

Aboubakary Liongo amezungumza na mwenyekiti na mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo ya easy finance Issack Kassanga.