1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen yarejea katika nafasi ya nne

9 Machi 2015

Bayer Leverkusen imerudi katika nafasi ya nne baada ya kusajili ushindi wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Paderborn. Ushindi huo umewaweka Leverkusen katika nafasi ya kufuzu katika Champions League

https://p.dw.com/p/1EniC
Fußball-Bundesliga-Spiel SC Paderborn gegen Bayer 04 Leverkusen
Picha: Getty Images/Afp/Patrik Stollarz

Leverkusen wako sasa pointi moja nyuma ya Schalke na Ausgburg. Beki wa Leverkusen Simon Rolfes alikiri kuwa haukuwa ushindi rahisi "Ilikuwa kazi ngumu kwa sababu tulipata shida kuudhibiti mchezo lakini tukaimarika tu katika kipindi cha pili. Na tulikuwa na bahati hatukurudi nyuma. Kwa bahati nzuri katika hali hiyo tukafunga moja bila. Hivyo tulifaulu na magoli yote yalikuwa mazuri" Paderborn sasa wako katika eneo la kushushwa ngazi, na watalazimika kutia bidii ili kusalia katika Bundesliga msimu ujao.

Katika mchuano mwingine wa jana, FC Cologne iliibamiza Eintract Frankfurt goli mabao manne kwa mawili. Ushindi huo umewapandisha hadi nafasi ya 11, pointi sita juu ya eneo la kushushwa daraja, wakati Eintracht wakiteremka hadi nafasi ya 9. Mkufunzi wa Cologne Peter Stöger aliwasifu vijana wake kufuatia ushindi huo "Tuna furaha kwa kushinda mechi hii. Tulikuwa na dakika 90 kupata kila kitu. Hata hivyo ilionekana katikakipindi cha pili. Frankfurt wana timu nzuri. Mambo yangekuwa tofauti lakini nadhani tulistahili kushinda leo".

Fußball-Bundesliga-Spiel 1. FC Köln gegen Eintracht Frankfurt
FC Cologne waliwazidi nguvu wageni FrankfurtPicha: Getty Images/Bongarts/Dennis Grombkowski/

Mabingwa Bayern Munich waliwazaba Hannover mabao matatu kwa sifuri siku ya Jumamosi na kupanua uongozi wao kileleni na pointi 11 baada ya nambari mbili Wolfsburg kushindwa bao moja kwa sifuri na Augsburg.

Schalke waliwanyamazisha Hoffenheim kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja. Borussia Dortmund walitoka sare ya bila na Hamburg na hivyo kusalia katika nafasi ya kumi. Roman Wiedenfeller ni mlinda mlango wa BVB "Tulipata pointi moja. Siyo rahisi kuja hapa Hamburg na kushinda hasa ikikumbukwa kuwa mara nyingi tumekuwa tukishindwa. Hivyo leo tulipata pointi moja muhimu".

Kwingineko, Werder Bremen walirejea katika mbinu za ushindi kwa kuwalaza Freburg bao moja kwa sifuri, na kuwaweka katika nafasi ya nane.

Borussia Moenchengladbach bado wako kwenye mkondo wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, wakiwa katika nafasi ya tatu baada ya kutoka sare ya 2-2 na Mainz. Naye kocha Mholanzi Huub Stevens angali kocha wa Stuttgart licha ya sare ya bila na Hertha Berlin ambayo iliwaacha wakishikilia mkia wa ligi

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman