1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya itanunua ndege 21 za Airbus kutoka Ufaransa

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZyk

Ufaransa na Libya zimetia saini mikataba ya kiuchumi yenye thamani ya takriban Euro bilioni 10.Kuambatana na mikataba hiyo,Libya itanunua ndege 21 aina ya Airbus na itasaidiwa kujenga mtambo wa nishati ya nyuklia.Mikataba hiyo imetiwa saini siku ya mwanzo ya ziara ya siku tano ya Rais wa Libya,Muammar Gaddafi nchini Ufaransa.

Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy ni kiongozi wa kwanza wa nchi ya Magharibi kumkaribisha Gaddafi, tangu kiongozi huyo wa Libya kulaani ugaidi na kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia hiyo miaka minne iliyopita.Hadi wakati huo,Libya kwa miongo kadhaa ilitengwa na jumuiya ya kimataifa. Lakini wanaharakati na Waziri wa Haki za Binadamu wa Ufaransa,Rama Yade wamekosoa ziara ya Gaddafi iliyoanza Siku ya Haki za Binadamu.