1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya kungali moto

18 Julai 2011

Mapigano yameshika kasi, kati ya vikosi vya waasi wa Libya na majeshi ya Muammar Gaddafi, kudhibiti mji wa mafuta Brega, mashariki ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/RaLZ
In this image made from television, a dust cloud is seen following the explosion of a missile, outside the strategic oil port of Brega, Libya, Thursday, April 7, 2011. An apparent NATO airstrike slammed into a rebel combat convoy Thursday, killing at least five fighters and sharply boosting anger among anti-government forces after the second bungled mission in a week blamed on the military alliance. (AP Photo/National Transitional Council in Libya via AP Television News
Mripuko nje ya mji muhuímu wa mafuta, BregaPicha: AP

Vikosi vya waasi vimesema kuwa vimefanikiwa kuingia mji huo lakini bado haukutiwa mikononi mwao. Mji wa Brega, unadhibitiwa na majeshi ya Gaddafi, tangu mwezi wa Aprili.

Ripoti zinasema, kiasi ya waasi 13 wa Libya wameuawa na takriban 200 wamejeruhiwa, tangu mapigano ya kuudhibiti mji wa bandari Brega, kuanza siku ya Alkhamisi.

Libyan rebels fire from a rocket launcher during an exchange of fire with pro-Gadhafi forces along the frontline at the outskirts of Brega, Libya, Monday, April 4, 2011. (Foto:Nasser Nasser/AP/dapd)
Vikosi vya waasi wa Libya nje ya mji wa BregaPicha: dapd

Wakati huo huo, upande wa magharibi waasi walifanikiwa kuvisukuma nyuma vikosi vya Muammar Gaddafi. Na hii leo, televisheni ya Libya pia imeripoti kuwa wilaya ya Tajoura, mashariki ya mji mkuu wa Libya, imeshambuliwa na ndege za jumuiya ya kujihami ya NATO.

Hayo ni mashambulio ya kwanza kufanywa na NATO, karibu na mji mkuu baada ya siku kadhaa. Ripoti hiyo imesema kuwa mashambulio hayo yalilenga vituo vya kiraia na kijeshi, lakini haikueleza zaidi kuhusu vituo hivyo wala haikutaja kama kulikuwepo majeruhi.