1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya, Ufaransa zatiliana saini mkataba wa mabilioni ya fedha

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaBF

PARIS.Ufaransa na Libya zimetiliana saini mikataba mbalimbali yenye thamani ya kiasi cha euro billioni 10 katika siku ya kwanza ya ziara ya kiongozi wa Libya Muhammar Gadaffi nchini Ufaransa.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais Nicolaus Sarkozy wa Ufaransa, imesema kuwa mikataba hiyo ni pamoja na Ufaransa kuiuzia Libya ndege 21 za abiria aina ya Airbus na makubaliano ya ushirikiano katika nishati ya nuklia kwa matumizi ya kijamii.

Sarkozy ni kiongozi wa kwanza wa nchi za magharibi kumwalika kanali Gadaffi toka kiongozi hiyo alipotangaza kuacha kuunga mkono ugaidi na mpango wa kutengeza silaha za nuklia miaka minne iliyopita.

Kabla ya hapo Libya ilikuwa imetengwa na jumuiya ya kimataifa kwa miongo kadhaa.

Makundi ya haki za binadamu pamoja na waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya haki za binaadamu, Rama Yade wameshutumu ziara hiyo ya Kanali Gadaffi nchini Ufaransa ambayo ilianza katika siku ya maadhimisho ya haki za binanadamu duniani.