1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Israel ataka Afrika isaidie katika mgogoro wa mashariki ya kati.

Abdu Said Mtullya3 Septemba 2009

Waziri wamambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman atoa mwito kwa Afrika, isaidie katika mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/JOJT
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman anafanya ziara barani Afrika.Picha: AP

Waziri  wa  mambo  ya nje  wa  Israel Avigdor Lieberman  anatarajiwa kuwasili nchini Kenya leo jioni  kuendelea  na  ziara ya nchi  tano  barani  Afrika.

Waziri  huyo  alienza  ziara  hiyo nchini Ethiopia  amelitaka  bara la  Afrika   lisaidie katika  juhudi  za kuutatua   mgogoro wa mashariki  ya  kati.

Waziri Lieberman  amesema kutokana    na uhusiano wake  na  nchi  za kiarabu,   Afrika inaweza  kutoa  mchango  muhimu   katika mashariki  ya kati.

Waziri Lieberman amesema  Israel inaitarajia Afrika  isaidie  katika kuleta  mtazamo  wa ukadirifu na kuleta  maridhiano  katika mashariki ya kati. Ameeleza  kuwa  ,kutokana na uhusiano  wa nchi  za Afrika  na nchi  za Kiarabu  iwe katika  medani ya Umoja  wa nchi  za kiarabu  au  Umoja  wa nchi za Kiislamu-IOC,Afrika  inaweza  kuwa  na ushawishi  muhimu.

Waziri  Lieberman  ametoa mwito  huo muda mfupi tu  baada  ya kiongozi  wa   Libya Muammar  Gaddafi- mwenyekiti   wa sasa wa Umoja  wa  Afrika  kuzitaka  nchi  za Afrika  zizifunge balozi za Israel .

Gaddafi  aliwaambia  viongozi  wa nchi  za Afrika kwenye  mkutano wao  wa  kilele mjini  Tripoli  kwamba  Israel  inachochea migogoro  barani  Afrika na kwa hiyo  balozi zake zifungwe. 

Hatahivyo waziri  wa Israel  amesema harakati na maamuzi  ya  za nchi  za Afrika yanapaswa  kuonyesha  mtazamo  wa kujenga.

Amezitaka nchi  za Afrika  ziache  kuwa  na mtazamo  wa  kuegemea  upande   mmoja katika  maamuzi yao.

Waziri  wa mambo  ya nchi  za nje  wa Israel anafanya  ziara barani  Afrika  kwa lengo  la kuendeleza uhusiano  wa   kibiashara sambamba na kutafuta kuungwa  mkono kidiplomasia  katika  bara  ambapo pana mtazamo  thabiti  wa   kuziunga  mkono  nchi za  kiarabu.

Waziri  wa mambo ya  nje wa  Israel    bwana Lieberman  leo  anatarajiwa  kuwasilisi  nchini Kenya .

Katika  ziara  yake  barani Afrika  waziri huyo pia  atazitembelea,Ghana, Nigeria  na Uganda.