1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LILONGWE : Kituo cha tiba ya UKIMWI kwa watoto chafunguliwa

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwd

Malawi hapo jana imefunguwa mojawapo ya vituo vya kisasa kabisa vya tiba ya watoto wa maradhi ya UKIMWI barani Afrika kwa kile maafisa wanachosema kuwa ni hatua ya kwanza katika kupambana na janga hilo ambalo limeshuhudia watoto wengi wakipoteza maisha yao.

Waziri wa Afya wa Malawi Marjorie Ngaunje amesema Chuo Kipya cha Tiba ya UKIMWI kwa Watoto cha Kimataifa kitaleta matumaini kwa watoto wanaokadiriwa kufikia 83,000 nchini Malawi ambao hivi sasa wanaishi na vurusi vya HIV na UKIMWI.

Wakati akifunguwa kituo hicho katika mji mkuu wa Lilongwe waziri huyo amesema walikuwa hawana uwezo wa kushughulikia mahitaji magumu ya maelfu ya watoto wenye virusi vya HIV nchini Malawi lakini hivi sasa kituo hicho kitasaidia serikali kuongeza nguvu za harakati zake dhidi ya gonjwa hilo.