1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LILONGWE :Madonna kuzuru Malawi

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9b

Mwimbaji maarufu wa Marekani Madonna anatarajiwa kuzuru nchi ya Malawi kesho ikiwa ni miezi minane tangu kumpanga mtoto wa nchi hiyo David Banda.Babake wa kumzaa mtoto Yohane Banda anaripotiwa kumsubiri kwa shauku mwanawe vilevile Bi Madonna kwani walikutana kwa muda mfupi mahakamani.

Hii ni ziara yake ya pili anayonuia kuendelea na shughuli zake katika shirika lake la Raising Malawi nchini humo.

Yohane Banda anatarajiwa kukutana na mwananawe David katika nyumba ya yatima ya Home of Hope iliyoko eneo la Mchinji.David Banda aliishi katika nyumba hiyo kabla kuanza maisha yake mapya miezi minane iliyopita.

Bwana Yohane Banda ambaye ni mkulima alimepeleka mwanawe katika nyumba hiyo kufuatia kifo cha mkewe muda mfupi baada ya kujifungua.

Bi Madonna aliidhinishwa kwa muda na mahakama kuu kumpanga mtoto huyo kwa miezi 18 na kuruhusiwa kusafiri naye.Uamuzi huo ulisababisha mjadala mkali kuhusu sheria za kupanga watoto za Malawi kwani Ukimwi unasababisha mayatima wengi sana.Madonna kwa upande wake anakanusha kutumia pesa na nafsi yake katika jamii kuweza kumpata mtoto huyo kwa haraka.Kulingana na Yohane Banda babake mzazi David Banda,yeye aliidhinisha hilo ili kukwepa umasikini unaokumba nchi yake.