1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIMA: Polisi na wanajeshi kuzuia uporaji nchini Peru

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXm

Tetemeko jipya lililofuatilia likiwa na nguvu ya 5.5 kwenye Kipimo cha Richter limesababisha khofu miongoni mwa wakazi nchini Peru,ikiwa ni siku tatu baada ya tetemeko kubwa kuuwa kiasi ya watu 500 nchini humo.Tetemeko hilo jipya liliutikisa mji mkuu Lima pamoja na eneo lililoteketezwa na tetemeko la siku ya Jumatano,lililo umbali wa kilomita 300 kutoka Lima.

Wakati huo huo serikali imesema,itasambaza polisi 2,000 na wanajeshi 1,000 wengine katika miji mbali mbali ili kuzuia uporaji.Mji ulioathirika vibaya zaidi ni Pisco ambako umati ulivamia malori yaliyokuwa yakigawa chakula na maji.