1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIMA : Tetemeko lauwa watu 17

16 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYk

Watu 17 inaripotiwa kuwa wamekufa na sabini kujeruhiwa katika mji wa Ica baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Peru hapo jana.

Tetemeko hilo la kiwango cha richter cha 7. 9 lilitingisha majengo katika mji mkuu wa Lima na kuangusha nyumba kadhaa ndogo.Wafanyakazi walikimbia nje wakihofia kuanguka kwa majengo katika mji mkuu huo.

Tetemeko hilo lilipelekea kutolewa kwa onyo la gharika la tsunami kwa nchi nne za Peru,Chile,Ecuador na Colombia ambalo baadae liliondolewa.