1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIMASSOL,CYPRUS:Wanajeshi wa Ujerumani wamewasili Cyprus

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6L

Wanajeshi wa Ujerumani wamewasili hii leo Cyprus kuelekea katika pwani ya Lebanon ambako wataungana na kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa.

Meli nane zenye wanajeshi kiasi 1000 imetia nanga katika bandari ya mji wa Limassol.

Ujerumani inatuma jumlya ya wanajeshi wake 2,400 ambao kazi yao itakuwa ni kushughulikia tatizo la kuingizwa silaha kwa kundi la Hezbollah kama sehemu ya makubaliano ya amani ya Umoja wa Mataifa kati ya wapiganaji hao na taifa la Israel.