1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIPUNGA.sakata ya mtoto wa Malawi anayetarajiwa kulelewa na Madonna yazusha mvutano mpya

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD09

Baba wa mtoto anayetarajiwa kulelewa na mwanamuziki wa kimataifa Madonna kutoka nchini Malawi ameongeza mvutano mpya katika sakata hiyo iliyogonga vyombo vya habari duniani kote.

Baba huyo sasa anasema kuwa hakuwa na nia wala matarajio ya kumgawa mwanawe kwa mwanamuziki huyo ila makubaliano yalikuwa tu Madonna angemlea mtoto huyo kwa niaba ya baba huyo.

Ugeugeu huo umesababisha muelekeo mpya katika sakata inayo muhusu mtoto wa kimalawi ambae mwanamuziki maarufu duniani anatarajia kumlea na kumfanya mwana.