1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON : Mchakato wa amani Mashariki ya Kati kuanza tena

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgw

Wasuluhishi wa pande nne juu ya mzozo wa Mashariki ya Kati wamekuwa wakikutana nchini Ureno kwa mara ya kwanza kabisa na Tony Blair mjumbe maalum.

Kundi hilo la pande nne linajumuisha Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi.Kabla ya kuanza kwa mkutano huo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amesema alikuwa anaamini kwamba kuna shauku ya dhati kujaribu kuutatuwa mzozo kati ya Wapalestina na Israel.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Javier Solana hapo Jumatano alikuwako Ramallah Ukingo wa Magharibi ambapo alikutana na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina pamoja na waziri mkuu Salam Fayad.

Solana amesema anafikiri uwezekano uliopo hivi sasa wa kuchukuwa hatua kwa pamoja Israel na Wapalestina unazidi kuboreka na anafikiri msukumo mpya unaweza kuanzishwa na kwamba hiyo ndio sababu iliomfikisha huko kuona kuwa wanaweza kushirikiana ili kuufanya msukumo huo upige hatua.

Kwa upande wake ziara ya kwanza ya Tony Blair Mashariki ya Kati tokea awe mjumbe wa kundi la pande nne itaanza hapo Jumatatu wakati atakapokwenda Israel na Ukingo wa Magharibi.