1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Livni achaguliwa kuongoza Kadima

18 Septemba 2008

Waziri wa nje wa Israel Zipi Livni kuwa waziri mkuu mpya wa Israel.

https://p.dw.com/p/FKX1
Mofaz na Livni.Picha: AP

Waziri wa nje wa Israel Bibi Zipi Livni alichaguliwa jana mwenyekiti mpya wa chama cha KADIMA na hivyo amefunguliwa mlango wa kuwa waziri mkuu mpya wa Israel na wapili mwanamke tangu Bibi Golder Maier kushika wadhifa huo.

Bibi Livni atajaza pengo linaloachwa na waziri mkuu wa sasa Ehud Olmert anaipanga kujiuzulu kutokana na kashfa ya rushua.

Mara tu kujulikana ushindi wake wa chupuchupu kuwa mwenyekiti mpya wa chama cha KADIMA,waziri wa nje Bibi Zipi Livni, hakupoteza wakati kutangaza nia yake ya kuunda haraka serikali mpya ya muungano .

"Hatua ya kwanza ni kukiunganisha chama cha Kadima.Nilikiwisha sema :Wale wote walionipinga si maadui bali ni washirika.Kwani, tulikuwa mashindanoni na sasa tumerudi kuwa pamoja na tunabidi kuimarisha serikali ya muungano na kuepusha kutoelewana."

Bibi Livni sasa anapanga kukutana na kundi la wabunge la washirika wa vyama walivyounda serikali pamoja .Amesisitiza KUWA anaunyemelea wadhifa wa waziri mkuu akitambua jukumu kubwa analoljitwika.

Alipoulizwa na waandishi habari serikali yake itachukua umbo gani,alikwepa kujibu moja kwa moja.

"Kile asmbacho leo sitafanya, ni kugawa madaraka.Kwa jinsi nilivyoendesha kampeni ya uchaguzi huu, mliweza klujionea kwamba ninaongoza siasa tofauti na .Sikuahidi kitu na kwahivyo, sianzi sasa kuahidi ."

Mpinzani wake katika kuania wadhifa wa mwenyekiti wa chama cha Kadima,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Schaul Mofaz,ameshammpigia simu Bibi Livni kumpongeza kwa ushindi wake .Na Livni akasema kuwa anamuhitaji Bw.Mofaz ili kuimarisha serikali. Mwanasiasa huyu wa kike mwenye umri wa miaka 50 ameshinda kinyanganyiro hiki cha kurithi wadhifa unaoachwa na waziri mkuu Ehud Olmert kwa kura chache tu.

Kwa wingi wa kura 1.1 % Livni alishinda si kwa zaidi ya kura 500 ili kumpiga kumbo mpinzani wake chamani Mofaz. Bw.Mofaz ,alijaribu hadi dakika ya mwisho kutia shaka shaka iwapo matokeo ya uchaguzi wa jana ni sahihi.

Wafuasi wa mkuu huyo wa zamani wa majeshi walidai kulikuwapo kasoro fulani katika baadhi ya vituo vya kupiga kura.

Wakadi kwamba baadhi ya matokeo yanapaswa kukaguliwa upya kabla matokeo rasmi kutangazwa.

Waziri mkuu wa sasa anaeacha madaraka Ehud Olmert ,alikwisha mpongeza Bibi Livni tangu jana usiku mara tu matokeo ya mwanzo kuashiria ushindi wake yalipotoka.

Alimuahidi kumsaidia katika kuchukua wadhifa huo mpya.