1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Livni na Netanyahu kila mmoja adai kushinda uchaguzi Israel

Aboubakary Jumaa Liongo11 Februari 2009

Mvutano wa nani mshindi katika uchaguzi mkuu wa Israel umejitokeza huku vyama viwili vya Likud na Kadima vikidai kushinda

https://p.dw.com/p/GrGp
Kiongozi wa chama cha Kadima Tzipi LivniPicha: AP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Tzipi Livni na Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu kila mmoja ametangaza kuwa ameshinda katika uchaguzi  huo mkuu  wa hapo jana.


Wakati ambapo asilimia 91 ya kura zimekwishahesabiwa, vituo vya televisheni vya nchi hiyo vimesema kuwa chama cha Kadima cha Bi Livni kinaongoza kwa viti viwili dhidi ya kile cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu.


Lakini Waziri huyo mkuu wa zamani wa Israel akiwahutubia wafuasi wa chama chake amesema kuwa ana hakika ataongoza serikali ijayo.


Kwa upande wake Bi Livni aliwaambia wafuasi wake kuwa chama chake cha Kadima kimeshinda na kumuomba Netanyahu kujiunga naye katika serikali ya umoja atakayoingoza.


Matokeo rasmi yanategemewa kutangazwa  baadaye hii leo.