1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lobi ya silaha Marekani

13 Januari 2009

Lobi ya silaha Marekani kabla Obama kuingia Ikulu

https://p.dw.com/p/GWi9
Rais George Bush akaribia kumaliza muda wake.Picha: AP

"Cowboy" anaacha madaraka na "mwanadiplomasia" anaingia madarakani.

Januari 20,rais George Bush wa Marekani, atamkabidhi wadhifa wake rais-mteule Barack Obama-rais wa kwanza mweusi wa Marekani ambae ulimwengu mzima, unataraji atarekebisha kila kitu kiwe bora kuliko ilivyokuwa wakati wa mtangulizi wake. Kuna kikundi chenye nguvu nchini Marekani ambacho kina matarajio tofauti kabisa na hayo.Isitoshe, kikundi hicho kina hofu kubwa kwa rais mpya:Viwanda vya silaha vya Marekani.Ndio maana kabla kuingia madarakani kwa Obama, wafanyabiashara ya silaha, biashara yao imestawi mno kuliko ilivyotazamiwa.

Viwanda vya silaha ni tawi pekee ambalo siku chache kabla kutawazwa kwa rais mpya, biashara yake inastusha jinsi inavyostawi. Viwanda vya silaha havimudu hata kuunda silaha za kutosha..

Uchunguzi wa maoni miongoni mwa wanaomiliki silaha nchini Marekani , unaonesha Wamarekani wengi wa tabaka la wahafidhina wanahofia chini ya utawala wa Obama na kwa ajili ya wingi mkubwa mno wa chama cha Democrat katika Bunge la Marekani (Congress), ununuzi wa silaha kuanzia sasa utadhibitiwa barabara.

Rais-Mteule Barack Obama katika kampeni yake ya uchaguzi, alisisitiza kuziunganisha fikra mbili: Upande mmoja, ile haki ya kumiliki silaha inayohifadhiwa kikatiba na kwa upande wapili, kuwadhibiti bora zaidi wafanyabiashara ya silaha na wanunuzi wa silaha ili isiselele kuwa kila mwaka maalfu ya raia wa marekani wanauwawa kwa kufyatuliwa risasi -miongoni mwao chipukizi.

Siku zijazo ihakikishwe kuwa, wafanyabiashara ya silaha hawauzi silaha kimagendo au kwa mlango wa nyuma mitaani,mitaa ambayo tayari itayari kutumia nguvu-alisisitiza Obama wakati wa mikutano kadhaa ya kampeni za uchaguzi.Akaongeza kamwe hakusudii kuzinyakua silaha zilizonunuliwa kihalali .

Hatahivyo, wafanyabiashara wengi wa silaha ,wanahofia kimsingi Obama anapinga watu kumiliki silaha na kwamba msimamo wake hasa juu ya swali hili ni kutokana na mbinu za uchaguzi hakubainisha dhahiri.

"linda uhuru wa kumiliki silaha", "mshindeni Obama"-hiyo ndio iliokuwa risala ya kikundi cha LOBI ya silaha chenye nguvu mno Marekani tena muda mfupi kabla siku ya uchaguzi Novemba 4,mwaka jana. Athari za kampeni hii,hazikuchelewa kuonekana.Tangu wakati huo, imekuwa dhahiri kwamba Barack Obama sie mtu anaeingia Ikulu mwenye kuwaungamkono kwa moyo safi wapendao kumiliki silaha.Hii ikapelekea wapenzi wa bunduki na bastola kununua kwa wingi madukani .

Sasa wanabiashara wengi na wanaomiliki silaha, wanahofia kwamba Obama kama rais wa zamani Bill Clinton, atajaribu kupiga marufuku biashara ya bunduki na hasa kudhibiti zile zinazoitwa "gun shows".

Kwani, katika maduka ya silaha kama hizo, watu binafsi wanaweza bila kudhibitiwa kuuza maboma yao ya silaha walizorundika.Katika maduka ya kawaida ya kuuzia silaha,kuna orodha ya kubidi kungoja kwanza kabla hukununua ili uchunguzwe iwapo huna madhambi.

Tangu ilipobainika kuwa Barack Obama anakuwa rais wa Marekani,idadi ya uchunguzi wa shirika la Upelelezi la FBI wa wanunuzi wa silaha za aina hii na juhudi za kutaka kuzinunua, umepanda kwa kima cha 42 %.