1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Afikishwa mahakamani kujibu shtaka la shambulio la bomu.

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkv

Daktari mmoja mwenye asili ya Iraq amefikishwa mahakamani mjini London kwa madai yanayohusika na jaribio la hivi karibuni la shambulio la bomu katika gari dhidi ya uwanja mkubwa kabisa wa ndege nchini Scotland.

Bilal Abdullah , daktari mwenye umri wa miaka 27 mzaliwa wa Uingereza na kukulia nchini Iraq, anatuhumiwa kwa kuligonga gari lake lililokuwa limewekwa mitungi ya gesi ndani katika eneo kuu la uwanja huo wa Glasgow akiwa pamoja na mtu mwingine.

Wakili wa Abdullah, Mark Rackstraw amewaambia waandishi wa habari kuwa ni mapema mno kusema lolote hivi sasa.

Amesema Mark Rackstraw kuwa Bilal Abdullah anashtakiwa kwa kosa moja la kula njama za kutaka kusababisha mlipuko. Tunasubiri ameendelea kusema maelezo kamili ya upande wa mashtaka . suala hilo hivi sasa liko mbele ya mahakama na ni mapema mno kusema lolote kuhusu kesi hiyo hivi sasa.

Ni mtu wa kwanza kati ya watuhumiwa wanane kufikishwa mahakamani. Mapema jana Jumamosi , waziri mkuu Gordon Brown pamoja na mamia ya ndugu wa wahanga pamoja na watu walionusurika walijumuika katika maadhimisho ya mwaka wa pili wa kumbukumbu ya shambulio la July 7, 2005 la kigaidi dhidi ya mfumo wa usafiri wa mjini London ambapo watu 52 wameuwawa na wengine 700 walijeruhiwa.