1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Allan Johnston atunukiwa tuzo

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBln

Alan Johnston, mwandishi wa habari wa shirika la habari la BBC aliyeachiliwa huru jana baada ya kuzuiliwa na watekaji nyara kwa karibu miezi minne katika Ukanda wa Gaza, ametunukiwa tuzo mjini London.

Johnston mwenye umri wa miaka 45 ameshinda zawadi ya kila mwaka inayotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International inayotambua kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari katika kuripoti maswala ya haki za binadamu.

Jonston alikuwa amechaguliwa kwa zawadi hiyo katika uandishi wa habari wa redio kabla tangazo la kuachiliwa kwake kutolewa mapema jana.

Babake Johnston, Graham, aliichukua zawadi hiyo kwa niaba ya mwanawe kwenye sherehe iliyofanywa jana jioni katikakati mwa London.