1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Benazir Bhutto apanga kurejea Pakistan

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTi

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto amesema,bado hajapata makubaliano ya kugawana madaraka na Rais Pervez Musharraf,lakini anapanga kurejea Pakistan hivi karibuni.

Alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini London,Benazir Bhutto alisema,chama chake cha kisiasa nchini Pakistan,hapo tarehe 14 mwezi wa Septemba,ndio kitatangaza tarehe ya kurejea kwake.Akaongezea kuwa juu ya hivyo,yeye anafanya mipango yake,kurejea Pakistan.