1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Blair ataka jeshi lipelekwe Dafur

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIn

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair leo hii ameitaka dunia kuchukuwa msimamo mkali dhidi ya Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan na kusema kwamba wanajeshi wanapaswa kupelekwa nchini humo kuzuwiya kuenea kwa machafuko ya Dafur.

Akitetea dhima ya Uingereza katika vita vilivyoongozwa na Marekani nchini Iraq Blair amesema viongozi duniani inabidi wajiandae kuingilia kati popote pale wanapohisi kwamba usalama unatishiwa.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Sky amesema ageliichukulia Sudan msimamo mkali na kwamba wakati hafikiri kwamba wanaweza kutuma wanajeshi wao nchini humo jumuiya ya kimataifa inapaswa kupeleka wanajeshi wake.