1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Brown akataa ratiba ya majeshi kuondoka Irak

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVA

Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, amekataa miito ya kuweka ratiba ya kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni nchini Irak. Brown ameapa kwamba Uingereza itaendelea kutimiza wajibu wake kwa Wairaki na Umoja wa Mataifa.

Katika barua yake iliyochapishwa leo mjini London, Gordon Brown amesema Uingereza bado ina kazi muhimu ya kufanya nchini Irak na ina majukumu yaliyo wazi.

Matamshi ya waziri mkuu Gordon Brown yanaonekana kama juhudi ya kuwahakikishia walio na wasiwasi, hasa maafisa wa serikali ya Marekani, kwamba Uingereza inasita katika kujitolea kwake kwenye harakati za kijeshi.

Brown amekataa madai kwamba wanajeshi 5,000 wa Uingereza kusini mwa Irak hawana kazi kubwa ya kufanya na akasema bado wanauwezo wa kupambana na wapiganaji na kulinda usalama.