1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Brown atazamia kuongoza tofauti na Blair

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnf

Gordon Brown amepokea madaraka ya waziri mkuu wa Uingereza kutoka Tony Blair.Brown,aliekuwa waziri wa fedha,amekubali mualiko wa Malkia Elizabeth wa Pili,kuunda serikali mpya,baada ya kuwa na mkutano wa saa nzima katika kasri la Buckingham. Baadae Brown akahamia makao rasmi ya waziri mkuu yalio Downing St. Namba 10.Alipowasili katika makao yake mapya,Brown aliwaambia waandishi wa habari kuwa atajitahidi kama awezavyo.Amesema, hiyo ni ahadi yake kwa watu wote wa Uingereza na sasa ndio ianze kazi ya mageuzi.

Waziri mkuu mpya Brown anatazamiwa kulitaja baraza lake la mawaziri baadae hii leo.