1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Dakake Margaret Hassan awatolea mwito waislamu wadai maiti

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeJ

Dadake Margaret Hassan, muingereza aliyekuwa akifanya kazi na shirika la misaada na aliyetekwa nyara na kuuwawa nchini Irak miaka miwili iliyopita, amewataka waislamu waudai mwili wa marehemu kufuatia kunyongwa Saddam Hussein.

Deirdre Fitzsimons amevunjika moyo kuona kwamba waislamu wengi wamekasirishwa na hatua ya Saddam kunyongwa wakati wa siku kuu ya Eid al Adha, lakini hawakusema lolote dadake alipouwawa wakati wa mwezi wa ramadhani.

Margaret Hassan aliishi Irak kwa miaka 30 kabla kutekwa nyara mnamo mwezi Oktoba mwaka juzi na kuuwawa kwa kupigwa risasi mwezi mmoja baadaye.