1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Kamanda mkuu mpya wa majeshi ya Uingereza Jenerali Richard Dannatt ataka majeshi ya nchi yake yaondolewe kutoka Irak

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3M

Kamanda mkuu mpya wa majeshi ya Uingereza Jenerali Richard Dannatt ametaka kuondolewa haraka kwa majeshi ya nchi hiyo kutoka Irak.

Jenerali Dannatt ameelezea kuwa kuwapo kwa majeshi ya Uingereza nchini Irak kunaifanya hali ya usalama ya nchi hiyo iwe mbaya zaidi.

Jenerali Dannatt ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu katika jeshi la Uingereza kutoa kauli ya uwazi, kuikosoa sera ya nje ya serikali yake.

Serikali ya waziri mkuu Tony Blair haikusema chochote kuhusu matamshi hayo. Uingereza ina wanajeshi kiasi ya 7,000 nchini Irak katika kikosi cha majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani. Wanajeshi 119 kutoka Uingereza wameshauawa tangu kuingia nchini Irak mwaka wa 2003 kuuangusha utawala wa rais Saddam Hussein.