1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Kichekesho Ufaransa kuihukumu Rwanda

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCm8

Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye yuko katika mzozo mkali na Ufaransa juu ya kile kilichochochea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 amesema hapo jana ni kichekesho kwa serikali ya Ufaransa kutolea hukumu matukio katika nchi ya Afrika.

Rwanda ilivunja uhusiano wake wa kibaloszi na Ufaransa mwezi uliopita kupinga wito wa hakimu wa Ufaransa wa kutaka Kagame ashtakiwe kutokana na mauaji ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana tukio ambalo linaaminika kuwa ndio lililochochea mauaji ya kimbari ya nchi hiyo.

Tuhuma hizo ziliikasirisha serikali ya Kagame ambayo inaziita kuwa ni kisingizio cha kuficha ukweli wa dhima ya Ufaransa katika kuwafunza wanajeshi wa Rwanda waliofanya mauaji hayo kimbari.

Kagame ameliambia jopo la watu wenye busara la Chatham House mjini London kwamba hawakutilii mashaka kuhusika kwa Ufaransa kwenye mauaji hayo.