1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Kipaumbele ni tatizo la kuongezeka joto duniani

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwI

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair wamekubaliana kuwa suala la kupambana na kuongezeka kwa joto duniani lipewe kipaumbele katika ajenda ya kimataifa. Baada ya mkutano wake na Blair mjini London, Kansela Merkel aliwaambia waandishi wa habari kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kuu ya karne ya 21.Waziri Mkuu Blair ameahidi kuisaidia Ujerumani katika juhudi zake, itakaposhika kwa mwaka mmoja,wadhifa wa rais wa kundi la madola yalio tajiri kiviwanda-G8 na pia wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita.