1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri sana mazao na watu wa Afrika.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxz

Ripoti iliyotolewa na kundi la mashirika makuu ya kutoa misaada ya Uingereza pamoja na mashirika mengine ya kimataifa inasema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta athari mbaya kwa watu na mazao katika bara la Afrika.

Ripoti hiyo inaonya kuwa wakati mifumo ya hali ya hewa inabadilikabadilika , na kusababisha ukame na mafuriko , matokeo yanaweza kuwa maafa makubwa katika usalama wa chakula.

Utafiti wa hivi karibuni wa kisayansi unaonyesha kuwa bara hilo liko katika kiwango cha nyuzi joto 0.5 zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 100 iliyopita.

Maafisa wa ngazi ya juu wa mazingira wanaonya kuwa kuna ufa mkubwa baina ya uelewa wa uongezeko la ujoto duniani na nia ya kulishughulikia suala hilo.