1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Mamia waokolewa kutokana na mafuriko

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgM

Wafanyakazi wa helikopta na mashua hapo jana wamewaokowa mamia ya watu walionasa kwenye mafuriko baada ya dhoruba kupiga Uingereza na kufurika miji na vijiji.

Madereva wamelala kwenye magari katika barabara kuu zilizonyeshewa na mvua kubwa wakati wengine wakijaribu kutafuta magari yaliotelekezwa kwenye barabara kuu hapo Ijumaa baada ya mvua kusababisha kusita kwa usafiri kwa muda mrefu.

Inakadiriwa kwamba hasara kutokana na mafuriko hayo inaweza kufikia mamilioni ya paundi fedha za Uingereza.

Pershore mji ulioko kama kilomita 200 kutoka kaskazini magharibi mwa London ndio ulioathirika zaidi.