1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Mpelelezi wa zamani wa Urusi alishwa sumu

21 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqc

Madaktari wanaomtibu mpelelezi wa zamani wa Urusi na mpinzani mkali wa serikali ya Urusi wamesema huenda akawa amelishwa sumu ya thallium aina ya sumu ambayo hutumika zaidi katika kuuwa panya.

Alexander Litvinenko anatapia maisha yake kwenye hospitali ya London na Ikulu ya Urusi imekanusha taarifa zinazodokeza kwamba imeamuru kuuwawa kwa Litvinenko. Tawi la kupiga vita ugaidi mjini London kwa wakati huu linashughulikia kesi hiyo.

Litvinenko amesema ameanza kuuguwa wakati akichunguza kesi ya mwandishi habari wa Urusi Anna Politkovskaya mpinzani wa Rais Vladimir Putin ambaye alipigwa risasi na kuuwawa nyumbani kwake mjini Moscow mwezi uliopita.