1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Mtu mmoja aliyekutana na Litvinenko nae mahututi.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClU

Suala la jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko limechukua mkondo mpya. Hivi sasa mmoja kati ya watu ambao walikutaka , mfanyabiashara Mrusi Dmitry Kovtun, anasemekana kuwa yuko mahututi akipambana na umauti baada ya kuugua kutokana na sumu ya miale mjini Moscow.

Hata hivyo wakili wake amekanusha ripoti hizo.

Kovtun alikutana na Litvinenko siku ambayo alianza kuugua na anaonekana kuwa ni shahidi muhimu katika kesi hiyo.

Maafisa wa afya nchini Uingereza wamesema kuwa wafanyakazi saba katika hoteli mjini London ambayo Litvinenko alitembelea wamekutikana na viwango vya chini vya miale.

Wakati huo huo waendesha mashtaka nchini Urusi pia wameanzisha uchunguzi wao juu ya kifo cha Litvinenko. Alizikwa jana mjini London.