1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Ndege ya abiria yaruhusiwa kuendelea na safari

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeV

Ndege ya abiria ya Ugiriki iliyokuwa njiani kutoka mjini New York Marekani ikielekea mjini Athens, imeruhusiwa kuendelea na safari yake baada ya kulazimika kutua katika uwanja wa ndege wa Shannon magharibi mwa Ireland leo alfajiri.

Msemaji wa uwanja wa ndege wa Shannon amesema polisi wameipekua ndege hiyo lakini hawakupata bomu lolote.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Olypmpic Airlines, iliyokuwa imewabeba abiria 183 na wafanyakazi 12, ilitua baada ya watu wasiojulikana kupiga simu na kusema mlikuwa na bomu la Saddan Hussein ndani ya ndege hiyo.