1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Nusu ya umma duniani itahamia miji mikubwa

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnh

Zaidi ya nusu ya umma wa bilioni 6.6 duniani,utakuwa ukiishi katika miji mikuu,ifikapo mwaka 2008.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu duniani-UNPF iliyotolewa siku ya Jumatano mjini London. Mkurugenzi-mtendaji wa UNPF,Bibi Thoraya Ahmed Obaid amesema,miji mikubwa duniani haina uwezo wa kuwa na idadi hiyo ya watu.Akaongezea kuwa ikiwa hakutokuwepo mipango inayofaa,miji itakabiliwa na vitisho vya umasikini mkubwa,itikadi kali za kidini,nafasi chache kwa vijana na vile vile haki za wanawake zitaathirika vibaya.

Wakati huo huo,waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani,Bibi Heiedemarie Wieczorek-Zeul alipozungumza mjini Berlin kuhusu ripoti hiyo alisema:

“Hakuna tatizo duniani ambalo hatimae halitofika hadi huku.Kwa hivyo ni muhimu kuona kuwa matatizo yatenzuliwa kule yanakotokea.“