1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Nyendo za mifugo ya wanyama marufuku

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcK

Uingereza imepiga marufuku usafirishaji wa mifugo ya n’gombe kondoo na nguruwe kwa taifa zima kufuatia mripuko wa kichaa cha n’gombe kwenye shamba moja kusini mwa nchi hiyo.

Waziri Mkuu Gordon Brown alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kamati ya dharura nchini humo ijulikanayo kwa jina la COBRA kwa njia ya simu hapo jana usiku kujadili gonjwa hilo.

Ofisi ya Brown imesema kwamba waziri mkuu huyo atarudi mapema kutoka kwenye mapumziko kuongoza mkutano mwengine wa kamati ya Cobra kwenye ofisi ya baraza la mawaziri leo hii.

Mripuko wa gonjwa hilo hapo mwaka 2001 ulipelekea kuchinjwa kwa mamilioni ya wanyama nchini kote Uingereza.