1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Pakistan yaonywa itafukuzwa Jumuiya ya Madola

13 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJV

Jumuiya ya Madola imeipa Pakistan siku 10 kurejesha katiba ya nchi na kuondosha hali ya hatari au itakabiliwa na kitisho cha kufukuzwa kutoka jumuiya ya madola 53.

Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo,Don McKinnon amesema,uanachama wa Pakistan utaahirishwa,ikiwa Rais Pervez Musharraf wa Pakistan hatotekeleza madai hayo hadi mkesha wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola.Mkutano huo umepangwa kufanywa nchini Uganda kuanzia Novemba 23 hadi 25.