1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Prince Harry kupelekwa jeshini Iraq

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPZ

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha kwamba Prince Harry ambaye yuko kwenye nafasi ya tatu ya urithi wa ufalme wa Uingereza atapelekwa nchini Iraq.

Prince Harry mwenye umri wa miaka 22 ni luteni wa pili katika kikosi cha Uingereza cha Blues and Royals ambacho kinatazamiwa kuwekwa nchini Iraq kwa kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi wa Mei.

Habari hizo zinakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Tony Blair kutangaza kwamba wanajeshi 1,600 kati ya wanajeshi 7,000 wa Uingereza walioko nchini Iraq watarudishwa nyumbani kutoka Iraq katika cha kipindi miezi michache ijayo.