1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Serikali ya Irak yapanga mazungumza na waasi

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqK

Serikali ya Irak itafanya mazungumzo na wawakilishi wa makundi ya waasi nchini Irak wiki ijayo, ikiwa ni katika juhudi za kukomesha machafuko yanaoikumba nchi hiyo. Habari hiyo imechapishwa na gazeti la Times la nchini Uingereza ikimkariri waziri wa mdahalo na maridhiano wa Irak, Akram Al-Hakim.

Mkutano huo wa siku moja utafanyika aidha tarehe 28 au 29 mwezi huu na kitakuwa chanzo cha mikutano mingine ijayo itakaofanyika nje ya Irak, aidha mjini Damascus- Syria au Amman-Jordan mwezi Disemba mwaka huu au Januari mwaka ujao.

Waziri huyo wa mdahalo na maridhiano nchini Irak, Akram Al-Hakim, amenukuliwa na gazeti hilo la Times kusema kwamba wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa waasi kupitia kwa watu wengine.

Mkutano huo kati ya serikali na makundi ya waasi, utahudhuriwa pia na waziri mkuu wa Irak, Nuri al-Maliki na maafisa wengine wakuu wa Irak. Wanadiplomasia kutoka Uingereza na Marekani na viongozi wa majeshi ya kigeni yalioko Irak walialikwa pia, daima kulingana na gazeti la Times la nchini Uingereza.

Mkutano huo ambao uliahirishwa mara tatu, hutoyashirikisha makundi ya kigaidi kama Al-Qaida au Jeshi la Mehdi la kiongozi wa kishiha Moqtad al-Sadr lakini utazungumzia pia swala la wanamgambo wa kishiha.