1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Shambulio la Marekani ni uhalifu

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIJ

Afisa mchunguzi wa vifo nchini Uingereza amehukumu kwamba shambulio la anga la Marekani ambalo limemuuwa mwanajeshi wa Uingereza nchini Iraq kilikuwa ni kitendo cha uhalifu.

Mchunguzi huyo amesema kifo cha mwanajeshi huyo wa cheo cha lensi koplo Matty Hull katika shambaulio la Marekani kwa msafara wake karibu na Basra hapo mwaka 2003 kilikuwa kinaweza kabisa kuepukwa.

Amesema kwamba ndege hizo zilikuwa haziko katika hatari na kwa hiyo tukio hilo haliwezi kuhalalishwa kuwa la kujihami. Serikali ya Marekani imesema katika uchunguzi wake wa tukio hilo imewaona marubani walikuwa hawana makosa ambao walidhani msafara huo wa Uingereza kuwa ni wa Wairaqi.

Mchunguzi huyo wa vifo na serikali ya Uingereza mara kadhaa wamekuwa wakishutumu serikali ya Marekani kwa kujaribu kuficha maelezo kutoka uchunguzi wa kifo hicho.

Hukumu ya mchunguzi huyo haibani Marekani kisheria.