1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Sharif kurudi Pakistan hivi karibuni

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWc

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan anayeishi uhamishoni Nawaz Sharif ameahidi kurudi nyumba hivi karibuni kuwania uchaguzi katika juhudi za kumn’gowa madarakani Rais Pervez Musharraf.

Sharif alikuwa akizungumza mjini London mara tu baada ya mahkama kuu nchini Pakistan kutowa hukumu dhidi ya serikali na kusema kwamba anaweza kurudi nchini humo.

Sharif anasema wanahitaji kulirudisha jeshi kambini na wataliweka wazi jambo hilo kwamba lazima kuwepo kwa utawala wa sheria nchini Pakistan ambapo katiba haina budi kuheshimiwa, mahkama iwe huru,vyombo vya habari viwe huru na kwamba hakumna mjadala juu kanuni hizo.

Sharif ambaye aliondoka Pakistan baada ya kuondolewa na Generali Musharraf katika mapinduzi ya kijeshi amesema huo ni mwanzo wa mwisho kwa hasimu yake Musharraf.

Sharif mwenye umri wa miaka 57 alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa makosa kadhaa ikiwa ni pamoja na kukwepa kulipa kodi na uhaini baada ya kupinduliwa kwake hapo mwaka 1999 ambapo muda mfupi baadae alikwenda kuishi uhamishoni nchini Saudi Arabia.

Bado haijulikani iwapo atakabiliwa na mashtaka hayo wakati atakaporudi nyumbani.