1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Sheikh wa itikadi kali anaweza kurudishwa Marekani

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG17

Mahkama ya Uingereza imepitisha hukumu kwamba sheikh wa itikadi kali za Kiislam Abu Hamza al-Masri anaweza kurudishwa nchini Marekani kukabilina na mashtaka ya ugaidi.

Hamza mzalia wa Misri hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka saba gerezani kwa kuwachochea wafuasi wake kuwauwa makafiri.Sheik huyo anatakiwa na serikali ya Marekani kujibu mshtaka 11 ikiwa ni pamoja na kujaribu kuanzisha kambi ya Al Qaeda huko Oregon Marekani.

Kurudishwa kwake Marekani itabidi kuidinishwe na waziri wa mambo ya ndani nchini Uingereza.