1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Shirika la ndege la Uingereza kuanza tena safari zake.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgz

Shirika la ndege la Uingereza limesema kuwa linalenga kusafirisha asilimia 95 ya wasafiri kwenda na kutoka katika uwanja wa ndege wa Heathrow kama ilivyopangwa leo Jumamosi.

Uwanja mkubwa kabisa wa ndege mjini London umefunikwa na ukungu kwa muda wa siku tatu, na kusababisha safari za ndege kukatishwa na mamia kwa maelfu ya wasafiri kukwama.