1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Tony Blair amthibitisha Gordon Brown kama mrithi wake.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC35

Waziri mkuu anayeondoka madarakani nchini Uingereza Tony Blair amemuidhibisha rasmi waziri wake wa fedha Gordon Brown kumrithi kama kiongozi wa chama cha Labour na waziri mkuu.

Akizungumza mjini London, Blair amesema kuwa anamuunga mkono kwa dhati Brown.

Hii inakuja wakati Brown amezindua rasmi kampeni yake ya uchaguzi mbele ya waungaji wake mkono mjini London.

Blair ametangaza siku ya Alhamis kuwa atajiondoa kutoka madarakani ifikapo Juni 27.

Amewaambia wafuasi wake kuwa licha ya utata mkubwa uliojitokeza kuhusu kuhusika kwa majeshi ya Uingereza katika vita vya Iraq, amekuwa kila mara akifanya kile alichohisi kuwa ni sahihi kwa nchi hiyo.

Baadaye leo Ijumaa , waziri mkuu anatarajiwa kukutana na rais anayeondoka madarakani Jacques Chirac na rais mteule wa Ufaransa Nicolas Sarkozy mjini Paris.