1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Tony Blair anusurika na kura bungeni juu ya sera za serikali yake nchini Irak

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCx7

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameshinda katika kura bungeni iofanyiwa mswada wa sheria wa kutaka kufanyike uchanguzi kuhusu sera za serikali yake juu ya vita nchini Irak. Wabunge 298 wamepinga huku 273 wakikubali. Mswada huo wa sheria ambao uliungwa mkono na chama cha upinzani cha konsevative pamoja na vyama vidogo vidogo vya Scottland na Wales, ulikuwa ukipendekeza wabunge wazipitie sera za serikali ya Tony Blair kuhusu vita vya Irak.

Waziri wa Uingereza wa mambo ya kigeni Bibi Margaret Beckett, amesema kuna uwezekano kufanyike uchunguzi huo ila baada ya wanajeshi wa Uingereza kurudi nyumbani.