1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Tume inayochunguza kifo cha Litvinenko yapelekwa Urussi

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmc

Maafisa wa polisi nchini Uingereza wamesema,tume ya wapelelezi inayochunguza kifo cha Alexander Litvinenko kilichosababishwa na sumu,inapelekwa Moscow.Tume hiyo itazungumza na wale waliokutana na Litvinenko mjini London muda mfupi kabla ya jasusi huyo wa zamani wa Urusi kufariki hospitalini.Wakati huo huo,madaktari mjini London wanaendelea kuchunguza hali ya Mtaliana,Mario Scaramella,mtaalamu wa masuala ya usalama aliekutana na Litvinenko siku ile ile inayodhaniwa kuwa marehemu alipewa sumu. Scaramella alipofanyiwa uchunguzi,alionekana kuwa na polonium 210,iliyomuuwa Litvinenko,lakini yeye haonyeshi ishara za kuathirika na sumu hiyo. Litvinenko alipokuwa mahtuti kitandani,alishutumu kuwa rais Vladimir Putin aliamuru kifo chake, madai yaliyokanushwa vikali na serikali mjini Moscow.