1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Ugonjwa wa midomo na miguu wachomoza upya Uingereza

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQQ

Kesi mpya ya ugonjwa wa midomo na miguu imegunduliwa katika shamba moja la mifugo,kusini mwa Uingereza.Maafisa wamethibitisha kuwa shamba hilo lipo Surrey,kiasi ya kilomita 50 kutoka shamba lililoambukizwa ugonjwa huo katika mwezi wa Agosti.Kesi hii mpya,imetokea siku nne baada ya Uingereza kutangaza rasmi kuwa ugonjwa wa midomo na miguu umedhibitiwa nchini humo.