1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: uhusiano baina ya Uingereza na Marekani kuendelea kama ulivyo

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBij

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband amesisitiza kuwa uhusiano baina ya nchi yake na Marekani utaendelea kama ulivyo.

Waziri Miliband amesema hayo kufuatia kauli za mawaziri wengine wawili zilizoashiria kuwa uhusiano huo sasa umekuwa baridi.

Lakini bwana Miliband ameeleza kuwa hapatakuwa na mabadiliko katika mwelekeo wa waziri mkuu wa hapo awali bwana Tony Blair juu ya uhusiano huo.