1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza kuongeza vikosi vyake Afghanistan

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCP5

Uingereza inapanga kupeleka vikosi ziada nchini Afghanistan.Taarifa ya waziri wa ulinzi wa Uingereza Des Browne imesema,wanajeshi zaidi watakwenda Afghanistan lakini idadi yenyewe haitotangazwa mpaka siku ya Jumatatu.Hapo awali, vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuwa hadi wanajeshi 1,000 wengine watapelekwa Afghanistan.Idadi kubwa ya wanajeshi 5,000 wa Uingereza walio nchini Afghanistan wapo katika wilaya ya Helmand,kusini mwa nchi ambako kuna uwezekano wa kukabiliana na mashambulio mapya ya waasi pale barafu itakapoanza kuyayuka katika majuma machache yajayo.Wanamgambo wa Taliban wameapa kuwa wanajeshi wa kigeni nchini Afghanistan mwaka huu,watashuhudia mmwagiko mkubwa wa damu,tangu kupinduliwa kwa Wataliban mwaka 2001.